Esma Awa Mbogo Zari Kuteketeza Watoto

Esma Awa Mbogo Zari Kuteketeza Watoto
Esma Khan ambaye ni dada wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amegeuka mbogo kwelikweli baada ya mwanahabari wetu kumuuliza kuhusu madai ya aliyekuwa wifi yake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutelekezewa watoto na Diamond.  Paparazi wetu alitaka kujua kama familia ya Diamond inazungumziaje kauli ya Zari aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa Instagram alipokuwa anamjibu mmoja wa mashabiki wake aliyetaka kujua kama Diamond anamsaidia kulea watoto au la na ndipo mrembo huyo aliposema kuwa hapati msaada wowote.


Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Zari, Esma alifyatuka: “Sitaki kuulizwa habari hizo… unaniuliza mimi kwani zinanihusu? Kwani mimi ni Diamond, mambo ya ajabu ajabu… (tusi).”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad