MSANII wa filamu za Kibongo, Ester Kiama amewaponda mapedeshee wa mjini waliokuwa wakimwaga pesa kwa wanawake kuwa kwa sasa wamekuwa zilipendwa kwani mastaa wengi wanaangalia mapenzi na sio pesa zao tena. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Ester alisema mastaa wengi wamegundua mapenzi ya kweli hayapo kwa mapedeshee ambao walikuwa wanawatumia tu kupitia hela zao.
“Unajua zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika, wengi wa wasichana sasa hawatazami pesa bali mapenzi ya kweli na ndio maana ukichunguza utaona mastaa wanatoka na wanaume wa kawaida sana ambapo wakati mwingine si rahisi kuamini,” alisema Este
Ester Kiama Aponda Penzi la Mapedeshehe "Wanawake Sasa Hivi Wanamapenzi ya Kweli Awaangalii Pesa"
0
February 18, 2019
Tags