Fahyma wa Rayvanny Afunguka Kuitwa Yuda
0
February 16, 2019
MZAZI mwenzake na mkali wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ‘Mama Jayden’ amefungukia ishu ya kuitwa Yuda kwa sababu ya kuwa na urafiki na kila mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na akimuacha tu, naye anakata mawasiliano naye.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Fahyma amesema anashangaa kwa nini watu wanamuita Yuda wakati hayupo hivyo na hajawahi kugombana na mtu yeyote aliyeachana na Diamond. “Hivi watu wakoje jamani sasa u-Yuda huo vipi? Kwa hiyo walitaka Diamond akibadilisha msichana mwingine basi huyu wa sasa mimi nisiwe na urafiki naye kwa sababu nilikuwa na urafiki na X wake?
“Hivi watu wana akili kweli? Mimi uhusiano wa Diamond unanihusu nini mimi? Sina mamlaka ya kumchagulia mchumba Diamond hata akimuacha Tanasha akawa na mwingine pia tukikutana kwenye sherehe nitaongea naye vizuri na kupiga naye picha kama kawaida kwa sababu mimi mwenyewe ni mpenzi mtazamaji tu.
“Halafu kwanza huwa tunakutana kwenye event (hafla) tu, sijawahi kuwa na urafiki wa hivyo kama watu wanavyosema kwa hiyo waniache kabisa sitaki maneno jamani na mimi sio Yuda,” alisema Fahyma
STORI: Shamuma Awadhi, Dar
Tags