Frederick Sumaye Augua Ghafla Tanga na Kukimbizwa Hospitali

Frederick  Sumaye Augua Ghafla Tanga na Kukimbizwa Hospitali
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ameumwa ghafla akiwa Mkoani Tanga kwenye shughuli za Chama chake cha CHADEMA  ambapo yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene imesema amekimbizwa Hospitali ya Bombo na kupatiwa matibabu na inaelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.

“Mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi inafanyika” Amesema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano CHADEMA Tumaini Makene

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad