Godzilla Kuzikwa Leo Makaburi ya Kinondoni

Godzilla Kuzikwa Leo Makaburi ya Kinondoni
BAADA ya kifo cha ghafl a cha Msanii wa Muziki wa HipHop Bongo, Golden Mbunda ‘Godzilla’, kuleta mshituko mkubwa, leo Jumamosi saa 7 mchana anatarajiwa kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake, Godzilla aliwahi kutikisa tasnia hiyo kwa ngoma kali kama vile, Nataka Mkwanja, First Class aliyomshirikisha Mwasiti, Thanks God aliyomshirikisha Walter Chilambo, Stay, Nataka, KingZilla, Get High na Lakuchumpa.

Akizunguza mapema jana, msemaji wa familia hiyo baba mkubwa wa marehemu, Shida Msolwa, alisema mazishi ya mpendwa wao huyo yatafanyika leo saa 7 mchana kwenye Makaburi ya Kinondoni jiji Dar es Salaam.



Kabla ya taarifa hizi za maziko kutajwa, juzi dada wa marehemu, Joyce Mbunda, alisema marehemu Godzilla alifariki baada ya kushukwa na  presha iliyosababishwa na tatizo la kisukari mwilini.


Alisema, mdogo wake hajaugua kwa muda mrefu, isipokuwa usiku wa kuamkia Jamatatu baada ya kutoka matembezini alipitiliza chumbani kwake kulala ambapo alilala kwa muda mrefu tofauti na ilivyozoeleka, na alipoamka aliomba apewe barafu kwa madai alikuwa akijisikia vibaya. Baada ya kumpatia barafu hiyo na kunywa ghafl a alianza kutapika mfululizo ndipo wakaamua kumpeleka kwenye Zahanati ya Mico iliyopo maeneo ya Salasala na kufanyiwa vipimo ambapo aligundulika presha imeshuka na matatizo ya kisukari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad