Haji Manara amvaa vikali msemaji wa Yanga SC


Msemaji wa Simba SC, Haji Manara ameonyesha kuchukizwa vikali na tuhuma zilizotolewa na
msemaji wa Yanga SC, Dismas Ten kuwa Simba ilitumia mbinu chafu kuifunga Aly Ahly kutoka
Misri.

Hapo jana Msemaji wa Yanga SC, Disma Ten aliandika kwenye mtandao; 'Wasijifiche kwenye
kisingizio cha kumfunga Mwarabu, tabia yao ya kupuliza dawa vyumbani imeshajulikana,
hawatusumbui na safariii hawatoki'

Sasa Haji Manara ameeleza kuwa mara baada ya mchezo wao wa hapo kesho, Dismas Ten
athibitishe tuhumpohizo kwani zinaichafua klabu yao yenye wanachama na wapenzi wengi.

"Kuna haja na hoja ya huyu mtu kuthibitisha beyond reasonable doubt (pasina shaka) kuwa Simba inafanya mambo hayo,tena uthibitisho huu uwe katika vyombo vya kisheria. Tunaukubali utani ila sio tuhuma za kutuchafua," amesema.

Haji Manara ameendelea kwa kusema, 'Hatutakubali kuchafuliwa kihuni huni na watu wasiojua maadili,miiko na kanuni za football. Tunamalizana nao kesho na baada ya hapo tutahitaji athibitishe hizo tuhuma," ameeleza'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad