Hakimu Aulalamikia upande wa mashtaka kwa Kuchelewesha Ushahidi Kesi ya Vigogo Simba

Hakimu Aulalamikia upande wa mashtaka kwa Kuchelewesha Ushahidi Kesi ya Vigogo Simba
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu , Thomas Simba ameulalamikia upande wa mashtaka kwa kuchelewesha usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange .

Aliyasema hayo jana baada wakati kesi hiyo ipokuwa mbele yake kwa ajili yakuendelea kusilikilizwa, lakini wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa(Takukuru), Leonard Swai alieleza kuwa hawana shahidi.

Na kwamba walifanya mawasiliano na shahidi waliyemtarajia atoe ushahidi na kuwa walikwisha muandaa lakini kilichotokea jana alipokuwa akifanya mawasiliano naye hakumpata na hajui kinachoendelea juu yake.

Baada ya Swai kueleza hayo, Hakimu Simba alisema kesi hiyo bado ipo nyuma sana na tulikwisha panga iendelee kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo yaani jana na leo lakini anashangaa kusikia shahidi hajapatikana.

Hata hivyo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi Mosi na 6, mwaka huu ambapo ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka utaendelea.

Aveva na Nyange wanakabiliwa na mashtaka mengine zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha hizo bila mamlaka ya Kamati ya Utendaji ya Simba, kujipatia pesa isivyo halali (Aveva) na utakayishaji fedha yanayowakabili wote, Aveva na Kaburu.

 Katika kesi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe anakabiliwa na mashtaka mawili, ya kughushi nyaraka na kuwasilisha nyaraka za uwongo yeye pamoja na wenzake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad