Hali yazidi Kuwa Tete Venezuela, Magari ya Misaada yazuiwa Mpakani


Vikosi vya Rais Nicolas Maduro vimezuia malori ya msaada kuingia Venezuela kwa kutumia mabomu ya machozi baridi na risasi, na kuua waandamanaji wawili.

Malori yaliyojazwa chakula na dawa kutoka Marekani kwa ajili ya Venezuela yalirejea kwenye maghala nchini Colombia baada ya wafuasi wa upinzani kushindwa kuvunja vizuizi vya wanajeshi, na kusababisha waandamanaji kadhaa kujeruhiwa.

Aidha, kutokana na kitendo cha Colombia kumuunga mkono mpinzani wa Rais Maduro, Maduro amevunja uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Colombia na kuwapa wafanyakazi wa ubalozi masaa 24 kuondoka nchini humo.

Guaido, ambaye mataifa mengi ya Magharibi yanamtambua kama kiongozi halali wa Venezuela, alizindua msafara huo wa msaada kutoka mji wa Cucuta nchini Colombia siku ya Jumamosi.

Upinzani ulitarajia kwamba wanajeshi wa Venezuela wangeshindwa kurudisha misaada hiyo inayohitajika kwa haraka zaidi nchini humo, ambapo idadi ya raia wanaokadiliwa kufikia milioni 30 wanahitaji msaada.

Hata hivyo, mpinzani wa rais Nicolasi Maduro, Guaido amesema kuwa ataendelea kumshinikiza Maduro aruhusu msaada uingie nchini na kwamba atatafuta njia nyingine, ambapo amesema kuwa atahudhuria mkutano wa kundi la mataifa ya kikanda la Lima mjini Bogota siku ya Jumatatu ambao utahudhuriwa na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad