Halima Mdee Anyimwa Dhamana

Halima Mdee Anyimwa Dhamana
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halime Mdee anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuhojiwa na kunyimwa dhamana.

Wakili wake, Hekima Mwasipu alisema Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema, amehojiwa kwa muda wa saa mbili na kunyimwa dhamana.

Amesema Mdee alipokea wito na mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni (RCO) leo kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano kutokana na kauli ya uchochezi aliyoitoa kwenye mkutano kata ya Mikocheni Februari 21.

"Polisi wamemhoji kwa masaa mawili kutokana na kauli aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni," amesema wakili Hekima.

Mdee ambaye alifika kituoni hapo saa tatu asubuhi alianza kuhojiwa saa 6:15 hadi saa 8:20 ambapo baada ya mahojiano hayo alinyimwa dhamana.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tusikubali Kuharibiwa Amani yetu na Usalama
    Kwa uchochezi na Utovu wa Nidhamu wa Wachache Hawa.
    Wahenga walisema samaki mkunje angali Mbichi….!!

    Na Usipo funzwa na Wazazi ….Ulimwengu Utakufundisha…!!!

    Tanzania yetu ni Salama na hizi Element Hatutozivumilia Kutuangamiza…

    Jeshi letu la Polisi linafanya Kai nzuri na Weledi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad