Harmonize aeleza sababu za kuiita EP yake Afro Bongo na sababu ya kutumia baadhi ya maneno yaliyo kwenye ngoma ya Dully sykes
0
February 26, 2019
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya muziki ya WCB iliyochini ya Diamond Platnumz, Harmonize amefunguka mengi kuhusu EP yake aliyoiachia ya Afro Bongo.
Akiongea na Mseto East Afrika kutoka nchini Kenya, Harmonize amefunguka kuhusu suala la kuiita EP yake Afro Bongo Harmonize amesema:-
“Kwa sababu muziki wetu wa Tanzania unaitwa Bongo Fleva na muziki wa kiafrika unatambulika kama Afro Beats kwahiyo nikaunganisha nikaita Afro Bongo kwa sababu muziki wote ni wa Afrika sio Tanzania tu”
Mbali na hilo Harmonize ameongezea suala la kwenda kuizindulia Afro Bongo yake nchini Nigeria na kusema kuwa
” Kwa kuwa muziki anafanya kwa ajili ya Afrika nzima na duniani kote kwahiyo hakuona tabu sana kwenda kuzindua Nigeria kwani hata Marekani angeweza tu”
Lakini pia kuhusu kutumia baadhi ya mistari iliyo katika ngoma ya Dully Sykes, amesema kuwa
” Siku narekodi ngoma yangu alikuja Dully Sykes studio na akaingiza mistari yake ya wimbo huo wa Handsome na kuniambia niitumie kwenye wimbo wangu wa Inama ambao nimewashirikisha Diamond Platnumz na Burnaboy kwahiyo niliona hii mistari ili iende vizuri ni bora aitumie msanii wa Kinigeria kwahiyo nikamuomba Burna Boya aweze kuitumia na baada ya kuitumia ilikaa sawa sana kuliko na mimi ningeitumia hiyo mistari ya Dully Sykes”
By Ally Juma.
Tags