Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itatoa uamuzi juu ya uhalali wa mweyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba iliyofunguliwa na kundi linalomuunga mkono katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo Jumatatu Februari 18, 2019 na Jaji Benhajj Masoud wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati atakapotoa uamuzi wa kesi inayohusu mgogoro wa wajumbe halali wa bodi ya wadhamini wa chama hicho.
Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2017 ilifunguliwa na mbunge wa Malindi (CUF) Ally Salehe anayetoka kambi ya Maalim Seif, anayewakilishwa na mawakili Mpale Mpoki na Fatma Karume; dhidi ya Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita).
Wadaiwa wengine ni wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho kambi ya Profesa Lipumba waliopendekezwa na kuidhinishwa na Rita, ambao ni Peter Malebo, Hajira Silia, Azizi Dangesh, Amina Mshamu, Abdul Magomba, Asha Suleimani, Salha Mohamed, Suleiman Issa and Musa Kombo.
Wengine ni wajumbe waliokuwa wamependekezwa na kambi ya Maalim Seif, walioenguliwa na Rita, ambao ni Abdallah Khatau, Joram Bashange, All Suleiman, Juma Muchi, Mohamed Mohamed na Yohana Mbelwa.
Mbunge huyo anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa wapi ni wajumbe halali wa bodi ya chama hicho kati ya makundi hayo mawili, kwa mujibu wa sheria na chini ya Katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 toleo la mwaka 2014.
Hatima ya Profesa Lipumba Na Maalimu Seif Ndani ya CUF Kujulikana Leo
0
February 18, 2019
Tags