HATIMAYE R Kelly Aachiwa Kwa Dhamana
0
February 26, 2019
Nyota wa R&B R Kelly ameachiwa huru kutoka Gerezani Chicago Marekani baada ya kulipa dhamana ya dola za kimarekani 100,000, msemaji wa idara ya Polisi ameeleza.
Siku ya Jana R Kelly alikana mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Wanawake wanne, watatu kati yao walikuwa ni watoto wakati wa uhalifu huo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 52 alionekana akiwa amevaa koti la samawati, hakuzungumza na waandishi habari aliposindikizwa kutoka gerezani na wakili wake.
Muimbaji huyo amekabiliwa na tuhuma za unyanyasaji kwa miongo kadhaa pasi kushtakiwa na amekana tuhuma zote za awali.
Msemaji wa idara ya Polisi Sophia Ansari amethibitisha kwamba R Kelly amelipa dhamana hiyo ya dola za kimarekani 100,000 ambayo ni 10% ya dhamana ya dola milioni moja iliyowekwa na Jaji mwishoni mwa wiki.
Tags