Hatma ya Dhamana ya Mbowe na Matiko Kujulikana Kesho

Hatma ya Dhamana ya Mbowe na Matiko Kujulikana Kesho
Mbivu na Mbichi kuhusu hatima ya dhamana ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko inatarajiwa kujulikana kesho March 1, 2019 katika Mahakama ya Rufani.

Mbivu hizo ni kuhusu uamuzi utakaotolewa na Mahakama hiyo kuhusu rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Hatima hiyo imejulikana wakati kesi ya Mbowe na wenzake ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Kelvin Mhina baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na wanasubiri taratibu za rufaa.

Baada ya kueleza hayo, Wakili Prof. Safari aliutaka upande wa mashtaka kueleza rufaa inaendeleaje kwani taarifa rasmi waliyoipata wao uamuzi wa rufaa hiyo utatolewa kesho February 29, 2019.

“Taarifa rasmi, rufaa itatolewa hukumu kesho Februari 29, 2019 saa tatu,”.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 14, 2019.

Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika.

Hata hivyo, baada ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu.

Rufaa ya (DPP) dhidi ya Mbowe na Matiko ilisikilizwa chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Stella Mgasha, Mwanaisha Kwariko na Gerald Ndika.

Mbali na Mbowe na Matiko, washitakiwa wengine katika kesi ya msingi iliyopo Kisutu ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad