Huku Simba Ikiwaliza Watanzania, Majirani Gor Mahia yainyoosha Zamalek


Mabinga wa ligi ya soka nchini Kenya Gor Mahia walionyesha umahiri wao kwa kutoka nyuma na kupata ushindi mkubwa wa 4-2 dhidi ya klabu ya Zamalek kutoka Misri katika kombe la Shirikisho barani Afrika Caf katika mechi ya kundi D iliochezwa katika uwanja wa michezo wa kasarani jijini Nairobi.

Mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuisenge alifunga magoli mawili huku Nicholas Kipkurui akiongeza bao jingine na kufanya mambo kuwa 3-2 huku naye Ibrahim Hassan akiwafungia wageni hao magoli mawili kabla ya Denis Oliech kuingia kama mchezaji wa ziada na kuipatia Gor Mahia ushindi mkubwa 4-2 baada ya kucheza kwa utulivu.

Kipkurui alipofunga goli lake la kwanza la kimataifa alilazimika kutolewa katika kipindi cha pili baada vya kupata jeraha na nafasi yake ikachukuliwa na Oliech ambaye aliwapatia mabeki wa Zamalek matatizo makubwa.

Ushindi huo unaiweka Gor ahia katika nafasi nzuri katika kundi hilo huku wakitafuta tiketi ya kufuzu katika robo fainali ya michuano hiyo.

Katika uwanja wa Kasarani, mashabiki wa Gor Mahia walijitokeza kwa wingi, wakiwa na hamu ya kuiona timu yao iklipiza kisasi cha mwaka 1984 dhidi ya Wamisri hao ambao waliisababisha K'Ogalo kufungiwa katika michuano hiyo kwa miaka miwili.

Hali ilionekana kuwa mbaya mapema kunako dakika ya saba wakati timu hiyo ya nyumbani ilipofungwa bao la mapema kufuatia makosa ya Boniface Oluoch. lkaini Tuyisenge alisawazisha baada ya dakika 27 kabla ya kufunga tena baada ya pasi nzuri kutoka kwa Francis Kahata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad