Ikiwa Imepita SIKU Moja tuu AZAM Kufukuza Makocha Wake..Warithi Watajwa


Baada ya Azam FC kuachana rasmi na Kocha wake Mkuu  Hans Pluijm pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi nafasi zao zitazibwa kwa muda na makocha wa timu za Vijana.

Maamuzi hayo yamekuja kwa makubaliano ya pande zote mbili kukubaliana kutokana na kutoridhishwa na matokeo yake ya hivi karibuni ya kwenye mechi za Ligi Kuu Bara (TPL).

Kwa taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam FC, sasa benchi la ufundi litakuwa chini ya makocha wa timu za Vijana, Meja Mstaafu Abdul Mingange (U20) na Idd Cheche (U17).

Kwa sasa Uongozi wa Azam tayari umeanza mchakato wa kumtafuta atakayerithi mikoba ya Kocha huyo raia wa Uholanzi.

Pluijm ameiongoza Azam FC kwenye michezo 25 na amepoteza michezo mitatu ameshinda 14 na kutoa sare nane akiwa na pointi 50 nafasi ya pili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad