Jeshi la Marekani kwa ushirikiano na utawala wa Libya unaoungwa mkono kimataifa limeendesha operesheni Kusini mwa Libya . Opereheni hiyo imetajwa kuwa walengwa ni magaidi wa kundi la al Qaida ambao wanajaribu kujikusanya katika eneo hilo.
Kulingana na mshauri wa uongozi wa Libya unaotambulika kimataifa Muhammed es Sallak, shambulizi hilo la anga limelenga kambi za magaidi wa al Qaida Ubari Kusini mwa Libya.
Mshambulizi kama hayo yamewahi kuendeshwa na jeshi la Marekani dhidi ya ngome za wangambo wa Daesh nchini Libya.
Ifahamike kuwa miaka minane inakaribia tangu kupinduliwa na kuuawa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na kuvamiwa na jeshi la Magharibi.
Jeshi la Marekani lashambulia kambi za al Qaida Kusini mwa Libya
0
February 15, 2019
Tags