Jeshi la Marekani lashambulia kambi za al Qaida Kusini mwa Libya

Jeshi la Marekani lashambulia kambi za al Qaida Kusini mwa Libya
Jeshi la Marekani  kwa ushirikiano na  utawala wa Libya unaoungwa  mkono kimataifa  limeendesha operesheni  Kusini mwa Libya . Opereheni hiyo imetajwa kuwa walengwa ni magaidi wa kundi la al Qaida ambao wanajaribu kujikusanya katika eneo hilo.

Kulingana na  mshauri wa uongozi wa Libya unaotambulika kimataifa Muhammed es Sallak, shambulizi hilo la anga limelenga kambi za magaidi wa al Qaida Ubari Kusini mwa Libya.

Mshambulizi kama hayo yamewahi kuendeshwa na  jeshi la Marekani dhidi ya ngome za wangambo wa Daesh nchini Libya.

Ifahamike kuwa miaka  minane inakaribia tangu kupinduliwa na kuuawa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na kuvamiwa na jeshi la Magharibi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad