Jose Mourinho Amehukumiwa Miezi 12 Jela Hispania



Kocha wa zamani wa Man United Jose Mourinho leo Jumanne ya January 5 2019 amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela na faini ya euro 182,500 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 480 kutokana na kutenda kosa la ukwepaji kodi nchini Hispania.

Jose Mourinho ameripotiwa kutenda kosa hilo akiwa anaifundisha Real Madrid wakati huo ila kosa lake la ukwepaji kodi wa haki za mauzo ya picha zake (images), alilifanya kati ya mwaka 2011 na 2012, hivyo Jose Mourinho kwa kosa hilo anaweza kukwepa kwenda jela kwa kulipa faini ya ziada ya euro milioni 1.98 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 5.2.

Sheria za nchini Hispania kama umetenda kosa na kukutwa na hatia Hispania kwa mara ya kwanza na kuhukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili utakuwa na uhuru wa kulipa faini na kuepuka kifungo jela, kocha Jose Mourinho mwenye umri wa miaka 56 aliwahi kuifundisha club ya Real Madrid mwaka 2010 hadi mwaka 2013
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad