Kagere Afunguka sababu ya Kuutafuta Mpira Kwenye Nyavu

Kagere Afunguka sababu ya Kuutafuta Mpira Kwenye Nyavu
Tunavyozungumza hivi sasa, Simba ipo mkoani Iringa kwaajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Lipuli FC, Jumanne katika uwanja wa Samora mjini humo.


Meddie Kagere, Clatous Chama na Zana Coulibaly wakiutafuta mpira kwenye mchezo dhidi ya Azam FC

Katika mchezo wa 'Matajiri wa Jiji' Simba na Azam FC uliopigwa Februari 23, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alifanya tukio ambalo lilizua gumzo mitandaoni baada ya kuutafuta mpira katika wavu wa Azam FC mara baada ya kuifungia bao la tatu timu yake katika dakika ya 78. Mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1.

Akizungumzia tukio hilo, Kagere amesema kuwa baada ya kufunga bao hakujua kama mpira umerudi uwanjani ama la, ndipo alipoamua kuutafuta huku wenzake wakimfuta.

"Unajua mpira ni burudani na ubunifu, sasa baada ya kufunga lile bao sikujua kama mpira utakuwa umerudi uwanjani ama umetoboa nyavu nikaanza kuufuata na wenzangu wakanifuata pia na ikawa ni burudani, ila ninashuru kwa matokeo tuliyoyapata", amesema Kagere.

Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, uongozi wa klabu ya Azam FC ulimtimua kocha wake mkuu, Hans van der Pluijm pamoja na kocha msaidizi, Juma Mwambusi kwa kile ilichodai kuwa ni kushtushwa na matokeo mabovu katka michezo takribani mitano ya hivi karibuni.

Katika msimamo wa ligi hivi sasa, Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 45, huku Yanga ikiendelea kusalia kileleni kwa pointi 61 na Azam FC ikiwa katika nafasi ya pili kwa pointi 50.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad