Kajala Afunguka Kuhusu Video Waliyokuwa Wanakata Mauno na Mwanaye Paula

Kajala Afunguka Kuhusu Video Waliyokuwa Wanakata Mauno na Mwanaye Paula
STAA wa Filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kuzungumzia video yake na mwanaye Paula Paul iliyozua gumzo mtandaoni kutokana na muonekano wao wa kucheza kwa kukata nyonga ambapo amefichua siri ya video hiyo kuvuja.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Kajala alisema kuwa video hiyo haikuwa na lengo baya kama watu wanavyomshambulia mitandaoni bali ilipigwa alipokuwa akicheza na mwanaye huyo kama kujifurahisha tu.



“Watu wanatakiwa kujua video hiyo haina ubaya na wala haijavujishwa na mimi wala Paula, siku hiyo nilikuwa nyumbani nimelala kwani nilikuwa naumwa kwa muda mrefu.

“Akaja Paula na rafiki yake msichana aliyekuwa akisoma naye akaniomba niamke ili nichangamke kidogo kwani alinionea huruma kwa kukaa kwangu ‘siriasi’.



“Basi tukaweka muziki tukawa tunacheza kama mama na watoto wake.

“Baada ya hapo yule rafiki wa Paula alirekodi video na kuitupia kwenye group la wanafunzi wa shuleni kwao na kuiwekea maneno kuwa anatamani kuwa na mama kama mimi.

“Hapo ndipo watu wakaanza kurushiana na mwisho ndiyo ikafika kwenye mitandao ambako imezua mjadala mbaya,” alisema Kajala.



Alisisitiza kuwa alikuwa akicheza na mwanaye kama mama na mwana na wala hakuwa na nia mbaya naye.

Video ya Kajala akicheza na mwanaye ilivuja wikiendi iliyopita kwenye mitandao ya kijamii watu walipoiona kila mmoja aliandika lake kutokana na mitazamo tofauti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad