ItKamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim ameagiza dereva wa gari lililosababisha ajali iliyoua watu 19 katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoa wa Songwe ashtakiwe.
Akizungumza katika eneo la ajali hiyo iliyotokea Februari 21 mwaka huu majira ya saa 3:15 usiku, kamanda Muslim ameagiza polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kupata chanzo cha ajali na hatua kuchukuliwa kwa dereva na mmiliki wa gari hilo.
Kikubwa kilichoshangaza umma baada ya kauli ya Kamanda Muslim, ni kwamba dereva huyo naye ni mmoja waliofariki, huku akitoa maagizo mengine ya kushuughulikiwa kwa haraka ili kupunguza kasi ya ajali za barabarani.
“Hata kama dereva wa gari hilo amefariki lakini ipo sheria inayotumika kumshitaki, na pia mmiliki wa lori hilo amekwishajulikana na askari wa usalama barabarani wanamfuatilia, ili naye aje ajibu tuhuma za kuruhusu gari lake kutembea barabarani likiwa bovu”, amesema Muslimu.
Wakati huohuo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Kheri Kagya amesema miili 17 ya watu waliofariki katika ajali hiyo imeshatambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao, na miwili bado inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mkoa huo.
Kamanda wa Polisi ataka marehemu ashtakiwe Kisa Hiki Hapa
0
February 25, 2019
Tags