Kampeni Kufungwa Leo Nigeria Uchaguzi wa Urais Kufanyika Jumamosi

Kampeni Kufungwa Leo Nigeria Uchaguzi wa Urais  Kufanyika Jumamosi
Alhamisi ndio siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi nchini Nigeria, siku ya jumamosi nchi hiyo itafanya uchaguzi wa urais. Nigeria ilifanikiwa kuingia katika uongozi wa Kidemokrasia miaka minne tu iliyopita licha ya matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo hivi sasa.

Kampeni za uchaguzi zikisindikizwa na tungo za muziki kutoka kwa waimbaji mbalimbali, Rais wa sasa na Mgombea Mohamud Buhari ameahidi kupeleka nchi hii katika hatua nyingine endapo atachaguliwa.

Buhari ndie alikua mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa nchi hiyo.

Mapema wakati akifungua kampeni zake mwaka jana alisema kuwa vita ilianza muhula wa kwanza nahitaji kuendelea.

''tunawajibika kuwa kazi tuliyoanza muhula wa kwanza, ya kuhakikisha mali za nchi na rasilimali zinakua na umuhimu kwa wananchi wa kawaida'' alisema Buhari.

Lakini kuna maswali juu ya Afya ya Buhari mwenye umri wa miaka 76, amekua akisafiri mara kwa mara kwenda London kwa matibabu ya ungonjwa ambao umewekwa siri.

Kuna wagombea wengine 72 wa kiti cha urais, lakini mshindani mkuu ni Atiku Aboubakar , ikiwa ni mara yake ya nne kugombea kiti hiko.

Anasifika kuwa mfanyabiashara mzuri, lakini suala la Rushwa wakati alipokua makamu wa rais linatia doa jitihada zake.

''katika uchunguzi wote uliofanywa dhidi yangu, kama mimi ni mla rushwa ama la, hakuna ushahidi uliopatikana, na kama kuna yoyote mwenye ushahidi ajitokeze, sijawahi kutuhumiwa kuhusu rushwa'' alisisitza Atiku Aboubakar.


Lakini kwa yoyote atakayekua mshindi wa kiti cha Urais, suala la kwanza kulitibu ni usalama. Katikati mwa Nigeria kuna mapigano ya wakulima na wafugaji na kusababisha mauaji kadhaa mwaka uliopita, na kusini mwa nchi hiyo kuna mashambulizi ya makundi ya kigaidi wakilenga vyanzo vya mafuta.


''tunahitaji Amani, tunahitaji usalama, lengo la kupiga kura ni kuchagua mtu ambaye ataleta Amani Nigeria, watu wanapata shida, kuna njaa, hakuna malazi wala shule''

Mbali na usalama, eneo la kusini wapiga kura wanasisita juu kupunguzwa kwa gharama za maisha.

''mimi nataka tupate chakula kwa bei nafuu, gharama ni kubwa mno, na kodi pia zishushwe'' alisema aisha, kijana anayetarajia kupiga kura siku ya jumamosi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad