Kangi Lugola aagiza mkurugenzi kampuni ya Ortello Business Cooperation(OBC) ya Falme za Kiarabu kukamatwa


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameagiza mkurugenzi wa kampuni ya wawekezaji kutoka falme ya Kiarabu ya Ortello Business Cooperation(OBC), Isack Mollel kukamatwa kwa tuhuma za kuwaingiza nchini  wafanyakazi wa kigeni bila kufuata taratibu.

Lugola ametoa agizo hilo leo Jumatano Februari 13, 2019  katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha.

Amemuagiza kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Longinus Ribishumbwamu kumsaka mkurugenzi huyo kabla hajamaliza ziara yake jijini Arusha.

Amesema mkurugenzi huyo alitakiwa kujisalimisha polisi tangu wiki iliyopita sambamba na wafanyakazi 10 wa kampuni hiyo, waliokuwa wameingia nchini kinyume cha sheria ambao tayari wamefikishwa mahakamani na kesi yao itatajwa tena Februari 22, 2019.

"Kazi ambazo walikuja kufanya wafanyakazi hao zinaweza kufanywa na Watanzania hivyo kisheria hawakupaswa kuja nchini kufanya bila kufuata utaratibu,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad