Mgogoro kuhusu umiliki wa eneo la mpaka wa bahari Hindi kati ya Kenya na Somalia umeongezeka baada ya Nairobi kuamua kukata uhusiano wa kidiplomasia na Mogadishu kufuatia madai kwamba Somalia imenadi maeneo ya mafuta yaliopo mpakani.
Siku ya Jumamosi jioni , Nairobi ilitangaza kuwa inamrudisha nyumbani balozi wake aliyepo Mogadishu Luteni Jenerali mstaafu Lucas Tumbo , ikidai kuwa uamuzi wa Somalia kupiga mnada eneo moja la mafuta mjini London wiki iliopita ni sawa na uchokozi dhidi yake na mali yake asili.
Vilevile Nairobi ilimrudisha nyumbani balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Nur na kuchochea zaidi kesi inayoendelea mjini The Hague kuwa mgogoro wa kisiasa kati ya Nairobi na Mogadishu.
ADVERTISEMENT
Matumizi mengine 6 ya simu yako usiyoyajua
Nyota wa filamu ya Empire 'aliwalipa raia wa Nigeria kumshambulia'
Hamaki baada uchaguzi kuahirishwa Nigeria
''Uchokozi wa kiwango hiki hautakubaliwa na Wakenya wote, pamoja na watu wasamaria wema wanaoamini sheria ya kimataifa mbali na hatua za kusuluhisha migogoro'', katibu wa maswala ya kigeni nchini Kenya Macharia Kamau alisema.
''Kwa kupuuza suluhu ya sheria za kimataifa kuhusu mipaka ama makubaliano ya kisiasa kupitia diplomasia , serikali ya Somalia imeonyesha wazi bado haijakomaa kisiasa'' , aliongezea katibu huyo.
Katikati ya mgogoro huo ni eneo lililopo ndani ya bahari Hindi lenye ukubwa wa mraba maili 62,000 .
Haijulikani ni taifa gani linalomiliki eneo hilo lakini linaaminika kumiliki kiwango cha juu cha mafuta na gesi.
Uchimbaji
Kenya inasisitiza kwamba mpaka huo unakwenda sambamba na laini ya latitude na tayari ilikuwa imeuza leseni za uchimbaji mafuta kwa makampuni ya uchimbaji madini katika eneo hilo kabla ya mzozo huo kuchipuka.
Katikati ya mgongano huo ni visima vya mafuta vilivyopewa kampuni za kigeni kwa muda.
Kenya sasa imedai kwamba uchimbaji wa mafuta katika eneo hilo umesimamishwa kwa muda kama ishara ya uhusiano mwema, lakini Somalia inasisitiza kuwa hiyo haitoshi.
Somalia vilevile inasisitiza kuwa mpaka wake unafaa kuwa sambamba na mpaka wake wa kusini.
Kesi ya Somalia na Kenya yasikizwa mahakama ya UN
ICJ yasema kesi ya Kenya na Somalia itaendelea
Jeshi la Kenya lakana kunufaika na makaa Somalia
Swala hilo liliwasilishwa katika mahakama ya kimataifa ya haki ICJ mnamo mwezi Aprili 2014 baada ya majadiliano kugonga mwamba.
Kenya ilikuwa imepoteza kesi hiyo hapo awali na kulazmika kuwasilisha kesi yenye uzito kubwa.
Wataalam wa baharini hapo awali wameonya kwamba Kenya huenda ikapoteza kesi nzima iwapo uamuzi wa hapo awali utarudiwa.
Hatahivyo Kenya iliendelea na swala hilo huku aliyekuwa jaji mkuu Githu Muigai akiliwakilisha taifa hilo mbele ya mahakama ya mjini Hague.
Visima vinayozozaniwa
Iwapo Kenya itapoteza kesi hiyo basi italazimika kuwachilia visima vyake vitatu kati ya 20 katika bahari hindi kwa Somalia.
Visima vinavyozozaniwa ni L-21, L-23 na L-24 . Swala nyeti la mgogoro huo kati ya Kenya na Somalia ni alama ya mpaka wa baharini.
Huku Somalia ikisistiza kuwa alama hiyo ya Mmpaka inapita katikati katika mpaka wa Kenya na Somalia, Kenya inasisitiza kuwa mstari huo unafaa kuwa sawa.
Mstari wa mpaka wa Somalia unaonyesha eneo lenye pembe tatu la baharini ambalo linamilikiwa na Kenya na ambapo visima hivyo vitatu vipo.
Nakala za mahakamani zilizowasilishwa zinaonyesha kuwa visima hivyo vitatu vilivyopo katika eneo hilo la pembe tatu vilipewa kampuni moja ya Kitaliano na serikali ya Kenya.
Katika kesi yake Somalia inataka mahakama hiyo ya Hague kutoa uamuzi kuhusu eneo hilo linalogawanya Kenya na Somalia katika bahari Hindi , ikiwa ni pamoja na eneo la bara lililo na zaidi ya maili 200.
Kenya nayo inasema kuwa makubaliano ya 2009 yalikuwa yamependekeza kwamba uamuzi wa mwisho wa keshi hiyo utafanyika baada ya kamishna wa UN kuhusu mipaka ya bara Afrika kuonyesha kiwango cha mpaka huo.
Kenya yamrudisha nyumbani balozi wake wa Somalia huku ikimfurusha yule wa Somalia nchini humo
0
February 18, 2019
Tags