Kilichomkuta Adriunus BAADA Kuvamia Msafara wa Rais


Adriunus Landnam (34), mkaazi wa Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingilia msafara wa Rais wa Zanzibar.

Adriunus ambae ni Mfaransa wa Swedzan House akiwa dereva wa gari yenye namba za usajili Z 724 FF  private  akitokea mjini kueleka shamba alipatikana akitenda  kosa hilo huko Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.

Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashitaka wa serikali Asma Juma Khamis, mbele ya hakimu Rauhiya Hassan Bakari, alidai kuwa mtuhumiwa  huyo alipatikana na kosa hilo  siku ya Jumatano ya Febuari 20, mwaka huu mnamo majira ya saa 03:30 asubuhi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa kuingilia msafara wa Rais ni kosa kinyume na kifungu  128 (2) (3) cha sheria namba 7 sheria za Zanzibar.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad