Kipenga cha Uchaguzi Chapuliza Nigeria

Kipenga cha Uchaguzi Chapuliza Nigeria
Mamilioni ya watu nchini Nigeria hatimaye leo wanashiriki uchaguzi mkuu baada ya shughuli hiyo kuahirishwa ghafla wiki moja iliyopita.

Wagombea wawili wakuu ni rais Muhammadu Buhari, 76, na naibu wa rais wa zamani Atiku Abubakar, 72.

Bw. Buhari anasema amejenga msingi thabiti wa ustawi wa jamii lakini mpinzani wake anadai miundo mbinu ya utawala haifanyi kazi Nigeria.


Yeyote atakayeshindi uchaguzi huu anakabiliwa na kibarua cha kushughulikia masuala ya uhaba wa umeme, ufisadi, tishio la usalama na mdororo wa uchumi.

Haijabinika matokeo ya uchaguzi yatatolewa lini - Huenda ikawa Jumatatu, Jumanne, ama baadae.


Karatasi ya kupigia kura ya wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2019
Kwanini Uchaguzi ulicheleweshwa?

Uchaguzi wa awali ulikuwa umepangiwa kufanyika Jumamosi ya Februari 16 lakini Tume huru ya uchaguzi (Inec) ikatangaza kuahirishwa kwa shughuli hiyo saa tano kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.

Tume hiyo imetoa sababu kadhaa ya kuchelewesha uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na jaribio la kuhujumu shughuli hiyo, changamoto za kiufundi na hali mbaya ya hewa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad