Kutokana na Simba kufungwa mabao 5-0 katika mechi ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema mechi ya marudiano inapaswa kuchezwa saa 8 mchana.
Ndugai alieleza kuwa kupoteza kwa Simba huko Misri ilisababishwa na hali ya hewa ambapo mechi hiyo ilichezwa majira ya saa 4 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kiongozi huyo amefunguka kuwa ili waweze kuwaangamiza Waarabu mapema basi inapaswa mechi hiyo ichezwe saa 8 wakati jua likiwa kali.
Ndugai alisema kucheza kwa muda huo kunaweza kuwanyima ari na morali waliyokuwa nayo Al Ahly kwenye mechi ya kwanza na kufanikiwa kuwapoteza kirahisi.
"Kule kwa wenzetu kulikuwa na baridi, sasa wakicheza hapa kwetu mechi itabidi ichezwe saa 8 ili tuweze kuwamaliza haraka" alisema.
Al Ahly zitakutana tena raundi hii ikiwa ni uwanja wa taifa February 16 2019.