Kiungo wa Arsenal Ramsey Amesaini Mkataba wa Pauni Elfu 400 kwa Wiki Kujiunga na Juventus

Kiungo wa Arsenal Ramsey Amesaini Mkataba wa Pauni Elfu 400 kwa Wiki Kujiunga na Juventus
Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa katika cha pauni £400,000 kwa wiki.

Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.

Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo.

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 12.02.2019
'Historia inaonyesha kazi ya Sarri ipo hatarini'
Cavani na Neymar kukosa mechi dhidi ya Man Utd
Atakuwa mchezaji wa Uingereza anayelipwa mshahara mkubwa.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka.

Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni £3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini.

Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa "atakasalia katika kumbu kumbu ya historia" ya mashabiki.

Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa"ataendelea kuwaunga mkono 100%".

Aliendelea kuandika : "Mlinikaribisha katika klabu hiyo nikiwa kijana mdogo na nimeshuhudia nyakati nzuri na mbaya.

"Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad