Baada ya kutangazwa kushuka kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe kutoka asilimia 14 hadi asilimia 11.4, wananchi mkoani humo wamedai kuwa huenda kiwango hicho kikapanda tena kwa kile walichokidai kuwepo kwa upungufu wa upatikanaji wa mipira ya kiume (Kondomu).
Image result for kondom mipira ya kiume
Hali hiyo inajiri siku chache baada ya Baraza la Madiwani katika halmashauri ya Mji Makambako kuwasilisha hoja ya upungufu wa kondom ambapo walimtaka Mkurugenzi kupitia Wizara ya Afya kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo.
Wakizungumza na mtandao wa Kituo cha runinga cha EATV, baadhi ya wananchi mkoani Njombe wamesema kutokana na jitihada za serikali juu ya kupambana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kuna haja serikali kuangalia namna ya kuongeza kinga muhimu.
Nao, baadhi ya wahudumu wa nyumba za kulala wageni na wafanyabiashara wa Kondomu wamesema ni miezi mitatu sasa tangu kuanza kuadimika kwa bidhaa hiyo jambo ambalo limepelekea wateja kuzifuata mbali na nyumba hizo za kulala wageni tena kwa bei kubwa.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Makambako, Ernest Kyungu ametolea ufafanuzi juu ya changamoto hiyo na kubainisha kuwa serikali mkoani humo inaendelea kulifuatilia.
Kondom Bado Kaa la Moto Njombe Zatafutwa Kila Kona
0
February 21, 2019
Tags