Jengo la Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, limeteketea moto zikiwa ni takribani siku sita kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Kwa mujibu wa msemaji wa tume hiyo, jengo hilo ambalo lipo katika Jimbo la Plateau liliteketea jana na kuunguza vitu vyote muhimu katika uchaguzi huo yakiwamo makasha na karatasi za kupigia kura.
Msemaji huyo alisema njama hizo ni kutaka kukwamisha shughuli hiyo ya upigaji kura, lakini akakaririwa na gazeti la This Day akisema bado ni mapema kuwatuhumu wahusika.
Uchaguzi huo mkuu unatarajiwa kufanyika Jumamosi hii Februari 16, 2019.
Katika hatua nyingine, Mshirika mkuu wa Rais Muhammadu Buhari katika uchaguzi huo, Nasir El-Rufai amewatishia raia wa kigeni akisema yeyote ambaye atajaribu kuingilia mchakato huo atarejeshwa nyumbani kwao akiwa ndani ya mfuko wa kuhifadhia maiti.
Nasir El-Rufai, ambaye ni Gavana wa Jimbo la Kaduna, alitoka kauli hiyo juzi katika mahojiano na Kituo cha Televisheni ya Taifa, ilipoanzishwa mada kuhusu jukumu la jumuiya za kimataifa katika uchaguzi huo.
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Nigeria, jengo la tume ya uchaguzi lawaka moto
0
February 12, 2019
Tags