KULA Vyakula Hivi Ili Kurudisha Heshima ya Ndoa Nyumbani Kwako..!!!


Tangawizi

Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na mmoja wa wanadoa hoa kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa bila kujua kuwa vipo vyakula tunavyokula vinavyoweza kuchangia chemistry ya miili yetu kuhusiana na suala la hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na :

KARANGA

Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system).Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri na kulifurahia.
Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.

TANGAWIZI

Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.
Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

PILIPILI

Kama tunavyojua chakula ambacho kimeungwa na pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka.

Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mguso wa hisia za raha.

Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamsha haraka hisia za mapenzi na pia usaidia mwili kuwa na hisia za haraka zaidi kwa kuguswa na kadhalika.

ASALI

Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.

Pia utafiti unaonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa na uwezo wa hamu ya tendo la ndoa.

MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.

Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.

Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homoni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo.

Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia, kutaka au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.

NAFAKA

Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.

Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.

Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.

Kula nafaka kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikishia afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

CHOCOLATE

Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati mwanamke au mwanaume anapofika kileleni (orgasm)

OYSTERS

Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.

Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.

SOYA

Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.

Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) hali inyomfanya mwanamke kufurahia tendo bila maumivu  wakati wa tendo la ndoa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad