Taarifa hii inaibua maswali mengi juu ya mahusiano kati ya WCB na muimbaji huyo wa Kwangwaru .Uongozi wa WCB haukutangaza kwamba Harmonize ataachia EP
Waswahili wana usemi usemao ‘Mwiba hutokea pale ulipoingia’. Kama Harmonize mwenyewe angetangaza kama nasitisha kuachia EP yake kutokana na sababu za kibiashara isingekuwa big ishu. Lakini mpaka WCB wanaingilia na kusitisha kutoka kwa EP hiyo inamaanisha kwamba hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Harmonize na uongozi wa WCB. Harmonize amejitengenezea ‘Empire’ yake ndani ya WCB.
Hakuna anayebisha kwamba kwa sasa Harmonize ni mkubwa sana kwa wasanii WCB ukimtoa Diamond. Tena sio mkubwa tu kimuziki bali hata kwa kipato hata rais wa label hiyo, Diamond alithitisha hilo.
Katika mazingira hayo huwenda pia kuna baadhi ya watu anawasikiliza zaidi na kuwashirisha baadhi ya mambo yake ndio maana kumekuwa kukitokea sitomfahamu kama ya ishu ya kutoka EP.
EP ya Harmonize ya AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi.
Kwa mujibu wa sentensi hii (hapo juu) iliyotolewa na Sallam inaonekana kuna kitu kinaendelea, kwani hiyo EP ya AfroBongo ilikuwa inatoka chini ya label gani?. Kauli kama hizi zinaacha maswali mengi kwa mashabiki wengi wa muziki namna Harmonize anavyoweza kutangaza jambo akiwa ndani ya kampuni bila mabosi wake kujua.
Mashabiki waushitukia mchezo
Baada ya vitu hivyo kutokea tayari kuna baadhi ya mashabiki wanatafsiri huwenda kukawa na tatizo kati ya Harmonize na uongozi wake. Soma maoni hapo chini.
Mahmoudahamad28 “Mnazingua mnasema itatoka week ijayo chini ya#wcb kwani b4 ilikuwa itoke chini ya nani??” Charlz_rick “@sallam_sk nahisi haya yote yalitakiwa kuangiliwa na uongozi mzima wa WCB kabla ya kutangaza tarehe kwa sabbu hii ni mara ya pili kuahirishwa”
Sumalito “Kwani kabla ilikua itoke chini ya lebel gani? harmonise c yupo wcb au saivi ana lebel yake. l.,” Kibokilo “Ambao tumejaribu kumuelewa boss na kuchukizwa na kiherehere cha harmonize tugonge like hapa,”