Kura Zinaendelea Kuhesabiwa Nigeria Huku DUNIA Nzima Ikiangalia Kinachoendelea



Kura za Uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali zimeanza kuhesabiwa nchini Nigeria, huku muda wa kupigia kura ukiongezwa katika baadhi ya maeneo kufuatia kucheleweshwa Jumamosi Alfajiri.

Mpinzani Mkuu wa Rais Muhammadu Buhari 76 ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar, 72.

Yeyote atakayeibuka mshindi atalazimika kuzungumzia swala la ukosefu wa Umeme, tishio la usalama na hali mbaya ya Kiuchumi.

Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika Wiki iliopita lakini ukacheleweshwa dakika ya mwisho kutokana na matatizo ya kimipango.

Rais Buhari alipiga kura yake nyumbani kwao huko Daura kaskazini mwa jimbo la Katsina, alipoulizwa iwapo atampongeza  mpinzani wake iwapo atashinda alisema 'nitajipongeza mwenyewe'.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad