IKIWA ni siku moja baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Simba, Azam FC imeamua kuvunja benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya kocha mkuu, Hans van Der Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Azam TV wameandika; “RASMI: Azam FC imeachana na kocha wake Mholanzi Hans van der Pluijm (pichani) pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi. Taarifa zaidi itafuata.”
Azam FC wameandika; “Tunawaomba radhi mashabiki kwa matokeo ya hivi karibuni, tunapitia kipindi cha mpito hivi sasa, tutarejea kwenye hali yetu ya kawaida kama mwanzo, cha muhimu kilichobakia kwetu hivi sasa ni kufanya vizuri kila…
Awali, Pluijm alisema anashangazwa na matokeo hasi anayopata hali iliyomfanya aamue kubadili mbinu na kukaa kikao na wachezaji wake ili atafute mbinu mpya zitakazomsaidia kupata ushindi. Pluijm alianza kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar kisha akapoteza kw Tanzania Prisons kabla ya jana kunyooshwa na mnyama uwanja wa Mkapa, pia alipata sare mbele ya Alliance,Coastal Union na Lipuli.
Pluijm ambaye jana alikubali kupoteza kwa kupata mabao mengi zaidi kuliko ilivyo kawaida yake katika michezo yake yote aliyocheza kwenye ligi ambayo ni 25 na alifungwa mabao 3-1 kwa mara ya kwanza.
“Kama utasema vijana wangu hawachezi hilo siwezi kukubali ila nadhani kuna kitu ambacho wanakosa kwa sasa, nimeanza kugundua ila kwa kuwa wao ndio wahusika nitakaa nao kisha nizugumze nao kwa ukaribu zaidi,” amesema Pluijm.
Licha ya kupoteza mchezo wa jana bado inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza michezo 25 sawa na Yanga ila imezidiwa pointi 11 na vinara hao wa ligi kwani wana pointi 61.