Lissu Afunguka Kuhusu Kurudi Tanzania

Lissu Afunguka Kuhusu Kurudi Tanzania
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amefunguka kuhusu kurejea nchini.

Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA akiwa katika ziara yake nchini Marekani amesema anapenda kurejea Tanzania ili kuendelea na mijadala ya Bunge ila kwa sasa hawezi kutokana bado hajapona.

"Napenda kazi ya Bunge, napenda mijadala ya Bunge, ninapenda nchi yangu lakini kwa sasa imekuwa nchini ya kutisha. Nasema nime-miss sana mijadala ya Bunge. Naamini iko siku nitarudi na kuendelea nayo kwa vile napenda sana mijadala," amesema Tundu Lissu.

Utakumbuka Septemba 07, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi
akitokea Bungeni Jijini Dodoma. Lissu alipatiwa matibabu ya mwanzo nchini Kenya kisha kuhamishiwa Ubelgiji. Kwa sasa yupo katika ziara Marekani mara baada ya kufanya hivyo nchini Ujerumani na Uingereza.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lizzu, Msaliti wetu anae jijengea mazingira ya kiukimbizi WA hiari.
    Jua bunge Si kazi ila NI uwakilishi na pindi ukipoteza sifa Jua bunge utalisikia kwenye Bomba kama Hamorapa na Steve umeelewa ndugu Lizzu.
    Mimi nnavyo kutathmini hufai HATA kwa senti ya maji.
    Na kama Nia na madhumuni NI kwenda kwa mabwana zako uliowaahidi kuwatetea kuchukua Mali asili zetu na jitto alihongwa Tofali LA Mali zetu.. Hapa KATIKA AWAMU HII WOTE mmebugi stepu.
    Kwa taarifa yako ndege zimeingia na Makinikia bado tumeyazuia na m300$ kwa taarifa yako Barrick watazitoa muda Si mrefu.
    MUNGU amlonde kipenzi chetu WA Tanzania JPJM na kukufifizeni mlegee nyie mahasidi

    ReplyDelete
  2. Msipotoshe Habari... Matibabu ya mwanzo alifanyiwa KATIKA Hospital ya Jijini DODOMA.
    Tafadhalini sahihisha. Na it was crucial treatment to save his life.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad