Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuna haja ya dereva ya Mbunge wa Singida Mashariki, Adam Bakari kueleza kwanini alipohisi kuwa wanafuatiliwa na watu wa siojulikana siku ya kushambuliwa kwa Lissu hawakuchukua hatua ya kulipeleka gari kituo cha polisi.
Kangi Lugoa ametoa kauli hiyo Jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema maelezo ya dereva huyo yanatia shaka, wanataka awaeleze mambo kadhaa yatakayosaidia uchunguzi wa tukio hilo.
“Kwa hali ya kawaida ni jambo la kushangaza risasi zote hizo wanasema 38, hata moja haikumpata dereva huyu,” amesema Lugola.
Kuhusu kuondolewa kwa CCTV Lugola amesema, “huu ni upotoshwaji mkubwa ambao unalenga kuwadanganya wananchi na kuwataka waichukie serikali yao na Rais John Magufuli na mimi kama waziri wa mambo ya ndani sitokubali,”.
“Wao ndio walikuwepo watuambie hawa waliompiga risasi ni wanawake au wanaume, ni wanene au wembamba, warefu au wafupi”, ameongea Lugola.