Maalim Seif amtuhumu Makamu wa Rais kupanga njama

Maalim Seif amtuhumu Makamu wa Rais kupanga njama
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif amemtuhumu Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd kupanga njama za kukwamisha kazi yake ya kukijenga chama

Ameyasema hayo leo Februari 4 wakati akifungua tawi jipya la chama hicho, Jimbo la Kitope kisiwani Pemba, ambapo kabla ya ufunguzi wake, Sheha wa eneo hilo alionekana kupinga kufanyika kwa shughuli hiyo.

"Tumeipandisha tena bendera yetu hapa katika tawi la Kitope, tena ni kwenye nyumba ya Katibu wa chama na kwa niaba ya chama naomba nichukue fursa hii kumshukuru. Lakini naambiwa bwana Sheha kachanganyikiwa kidogo, hataki kabisa shughuli ifanyike", amesema Maalim Seif alipopewa nafasi ya kuhutubia katika shughuli hiyo.

"Tunamwambia kuwa Pemba nzima tumetembea, tumeanza juzi Unguja, Tumbatu, Kaskazini A lakini huko kote vituko hivyo havikuwepo. Bila shaka si yeye, atakuwa ni Balozi Seif Ali Idd, kwasababu anaifanya yeye kuwa Mahonda hii ni yake, hii ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi, kila chama kina haki ya kufanya siasa sehemu yoyote ile Tanzania sasa leo inakuwaje mtu mmoja anazuia shughuli kufanyika", ameongeza Maalim Seif.

Katibu Mkuu huyo wa CUF amekuwa katika ziara mbalimbali za kukijenga chama chake hasa katika kisiwa cha Pemba ambako ndiko ngome kuu chama hicho ilipo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad