Makamu wa Rais asikitikia rufaa ya kina Mbowe

Makamu wa Rais asikitikia rufaa ya kina Mbowe
Makamu wa Rais wa Chama Cha Wanasheria ambaye pia ni Wakili, Dk. Rugemeleza Nshala amesema kwamba jambo lililotokea leo katika mahakama ya Rufaa kwenye usikilizwaji wa rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ni kukomoa na kuumiza.

Dk. Nshala amesema kwamba kesi nzima iliyopelekwa na warufani haina mashiko na kwamba wao upande wa serikali una haki ambayo wengine hawana.

"Hatuwezi kujenga na watu wanakomoa wenzao(sadist country). Hakuna mwanadamu hata mmoja miongoni mwa tulioko hapa anaeweza kumuongezea mwenzake mda wa kuishi hapa duniani, kwahiyo kushiriki kupoteza hata saa mmoja ya uhuru mwenzako huwezi kuilipa,kwa bahati mbaya hawa wametumia sheria vibaya kupoteza uhuru wa warufaniwa",amesema Dk. Nshala, Leo alipokuwa kwenye mahakama ya Rufaa.

"DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana".

Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi amedai leo Jumatatu Februari 18, 2019 mbele ya jopo la majaji watatu Stella Mgasha, Gerald Ndika, Mwanaisha Kwaliko wa Mahakama ya Rufani kuwa wanapinga uamuzi uliotolewa na Jaji Rumanyika katika rufaa namba 344 ya 2018 uliotolewa Novemba 30, 2018.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala amedai sababu za rufaa hiyo hazina mashiko hivyo aliomba Mahakama ya Rufani kuitupilia mbali rufaa hiyo.

Mbowe na Matiko wamerejeshwa Segerea mpaka Februari 19 Asubuhi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad