Makonda Awachana Mastaa Kisa Ommy Dimpozi "Leo Angekufa Mitandao Ingechafuka kwa R.I.P Ommy Leo Ametoa Nyimbo Wamekaa Kimya"

Makonda Awachana Mastaa Kisa Ommy Dimpozi "Leo Angekufa Mitandao Ingechafuka kwa R.I.P Ommy Leo Ametoa Nyimbo Wamekaa Kimya"
Mkuu was mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda ameamula kutoa ya moyoni kwa Wasanii na mastaa wengine Ambao wameonyesha Ukimya katika kusapoti nyimbo Mpya ya MSANII Ommy Dimpozi ambaye alikaa Kimya kwa muda mrefu Kutokana na maradhi yanayomsumbua kwa muda Sasa.

Kupitia ukrasa wake Wa kijamii Makonda Atoa hisia zake kwa Kusema Kuwa mwanzoni waliweza kumpost kwa wingi pale alipozushiwa Kifo lakini ameshangazwa kuona watu wanashindwa kumsapoti Baada ya kupona na kutoa nyimbo ya kumshukuru mungu.

"Ukitaka kujua watu walivyo wa Ajabu tazama Leo Ommy Dimpozi alikua mgonjwa Sana na ilifika hatua watu walitangaza Kuwa amekufa, Leo amerejea Tena Akiwa ametoa na nyimbo ya kumshukuru mungu wamekaa Kimya Kama sio wao waliokuwa wanapost kumwambia Apone. Angefariki tungeona mitandao imechafuka Leo R.I.P Ommy ooh umeenda bado tunakuitaji. Unafki Huu sijui utaisha lini tunapenda kutangaza misiba kuliko uponuaji" aliandika Makonda

Ommy Dimpozi alikua anasumbuliwa muda mrefi ambapo mwanzoni alipelekwa Afrika Kusini kwa Matibabu na Kujulikana amekula sumu ya kwenye chakula au kinywaji Ambayo ilimletea madhara makubwa ya Koo na Hivi karibuni amerejea Kutokana Ujerumani kwa Matibabu ambapo Hadi Sasa amerejea Nchini Akiwa na Hali nzuri.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad