Mama Ajifungulia Kwenye Ndoo Ya Maji Na Kuua Kichanga.
0
February 16, 2019
Na John Walter-Babati
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linamshikilia mwanamke wa mtaa wa Nangara Babati mjini, Ramla Omary (23) kwa kosa la kutupa kichanga katika shimo la kichuguu karibu na nyumbani kwako mara baada ya kujifungua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana ijumaa Februari 15.2019 na kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga inaeleza kuwa, kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alihisi uchungu kumuuma ndipo alipoamka na kuchukua ndoo yenye maji ambayo aliikalia kisha kujifungua kichanga hicho ambacho hata hivyo alifariki baada ya kukosa pumzi ndani ya maji.
Kamanda Senga amesema mtuhumiwa huyo anadai kuwa sababu ya yeye kumuua kichanga hicho ni ugumu wa Maisha aliokuwa nao.
Hata hivyo mwili wa Kichanga hicho umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mji wa Babati [MRARA].
Tags