"Mama Aomba Nyimbo za Mwanae Zipigwe Msibani" Godzilla


Mama wa marehemu Godzilla ameomba nyimbo za mwanae zipigwe katika msiba huu na kuacha kuweka nyimbo zingine ambazo zingemtia machungu zaidi ya kumkumbuka mtoto wake .

Mama huyo ambae amekuwa mwenye uchungu sana kwa muda wote na kuongea maneno yenye huzuni na huruma kubwa kwa kutokuamini kuondoka kwa mtoto wake anasema kuwa anajua kuwa kuna baaadhi ya nyimbo za mtoto wake  zina maadhi ya dini hivyo anaomba nyimbo hizo zipigwe katika msiba.

Mama anasema kuwa kuna nyimbo ambazo zilikuwa ziko studio bado lakini zilikuwa zinakaribia kutoka kwa sabab tayari mtoto wake alikuwa amesikiliza hivyo anaomaba kuzisikia tena.

Akiongea na waandishi, moja ya watu wa karibu wa God , anasema kuwa mama alikuwa akimwambia alikuwa akipelekwa studio na mwanae na alikuwa akimsikiliza baadhi ya nyimbo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad