Mama yake Godzilla alimuomba msaada Mwasiti


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mwasiti amesema kwamba kutokana na jambo hilo akawa karibu sana na familia ya Godzilla, na kushirikiana kwenye masuala mbali mbali.

“Ilikuwa benki mjini, Godzilla alikuwa amekuja na mama yake, akaniambia napenda unavyoimba, ningependa pia umshike mkono mdogo wako na yeye aishi katika mazingira mazuri na kufanya kazi, nikamwambia sawa, mama, kuanzia hapo tukawa karibu sana kama familia, tulikuwa tunaongea mambo mengi sana”, amesema Masiti.

Ikumbukwe kwamba Mwasiti ni mmoja wa watu ambao walikuwa karibu sana na Godzilla, na kuweza kufanya kazi pamoja huku wakiwa na mlengo ya kuachia album ya pamoja.

Godzilla amefariki dunia juzi Februari 13, na anatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi, Februari 16 katika makaburi ya Kinondoni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad