Mambo 14 yaliyozungumzwa na Msemaji Mkuu wa Serikali leo jijni Dodoma
0
February 05, 2019
Muungwana Blog, imekuwekea mambo 14 yaliyozungumzwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi na Waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Haya ndio mambo 14 yaliyozungumzwa na Msemaji Mkuu jijini Dodoma;
1. Niwatakie kheri ya mwaka mpya Watanzania wote ambao katika nafasi zao kwa namna moja au nyingine wameendelea kuiunga mkono Serikali kwa kulipa kodi, kuwa wazalendo na kuchapa kazi
2. Rais Dkt. Magufuli amekuwa akiipatia heshima kubwa nchi yetu kwa mapambano dhidi ya rushwa
3. Tanzania imeendelea kuwa na taswira nzuri na heshima kubwa miongoni mwa mataifa mbalimbali duniani
4. Benki ya TIB katika robo ya tatu ya mwaka 2018 imepata faida ya TZS milioni 842 kutoka hasara ya TZS bilioni 1.29 katika kipindi kama hicho, huku ikitegemea kuondoa kabisa hasara ya mwaka ifikapo Juni mwaka 2019
5. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imekusanya jumla ya TZS Bilioni 94.01 kutoka kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu katika kipindi cha Julai- Disemba 2018 na kuvuka lengo la kukusanya TZS Bilioni 71.4 katika kipindi hicho
6. Mwezi Disemba 2018 pekee mwaka jana TRA ilivunja rekodi ya mwaka mzima kwa kukusanya TZS Trilioni 1.63 ambazo ni kubwa kwa mwaka mzima wa 2018
7. kwa mujibu wa Takwimu za mpaka Disemba 31, 2018 ambayo ni nusu ya mwaka wa bajeti Serikalini,TRA ilikusanya trilioni 7.99 sawa na ukuaji wa 2.01%
8. Moja ya azma kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha utendaji bora, utoaji huduma bora kwa wananchi, kukusanya mapato lakini pia Serikali kupata gawio
9. Tunaamini mwaka 2019 ukuaji wa uchumi utafikia asilimia 7.2 na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa katika mataifa matano Afrika kwa uchumi unaokuwa kwa kasi na kuendelea kuwemo katika nchi 10 duniani
10. Mpaka sasa Viongozi wote wako Dodoma na wafanyakazi asilimia 86.2 ya watumishi wote wa wizara wamehamia Dodoma
11. Natoa wito kwa watendaji wa Serikali, isipokuwa kama habari imezuiwa kisheria, kwa sasa kutoa habari na kueleza utekelezaji wa ahadi tulizoziahidi ni takwa la kisheria
12. Mpaka sasa Viongozi wote wako Dodoma na wafanyakazi zaidi ya asilimia 86.2 ya watumishi wote wa wizara wamehamia Dodoma
13. Tarehe 15 mwezi huu tunakwenda kumkabidhi mkandarasi eneo la mradi wa kuzalisha umeme Bonde la Mto Rufiji, ili aanze kazi, hii ni katika muendelezo wa Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi ya watanzania
14. kwa nia njema natoa notisi ya mwisho kwa wamiliki wa machapisho ambao hawajahuisha leseni zao ifikapo Machi 1, 2019 wawe wamehuisha lasivyo hawataruhusiwa kuyachapisha tena
Tags