Mbunge wa Jimbo la Iramba, Mwigulu Nchemba ameruhusiwa kutoka hospitali hii leo kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatano, Februari 13 mkoani Iringa.
Mbunge huyo alikuwa akisafiri kutoka Iringa kuelekea Dodoma, wakati gari lake lilipopata ajali hiyo katika eneo la Migori moani Iringa, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma.
Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao,