Maneno ya RC Mwanri kwa DC wa Uyui 'asikutishe shetani na mama mkwe wake'


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, RC Mwanri amesema kuwa ameenda kwenye Halmashauri ya Uyui kumtia moyo Mkuu wa Wilaya hiyo, Gift Msuya kuhusu suala la ugawaji wa vitambulisho huku akimueleza kuwa asimugope shetani wala mama mkwe wake.

RC Mwanri amesema hayo alipotembelea Halmashauri hiyo anesema kuwa wananchi wasifikiri kuwa ana wasiwasi na wao ila amekuja kuwatia moyo kwakuwa Halmashauri hiyo ndiyo inaongoza

"Mkuu wa Wilaya nimekuja hapa kusahihisha mambo kufanya collection wala wananchi wa Wilaya ya Uyui msije mkafikiri nina wasiwasi na nyinyi Halmshauri ndio inaongoza kwa Halmashauri zote mkoa wa Tabora kwahiyo wazee msije mkasema sijui hapa naongea na wazee ninaojua wanaongoza darasani," Alisema RC Mwanri.

"Nimekuja hapa kuwatia moyo nimekuja kukwambia DC Msuya songa mbele sisi serikali tuko nyuma yako tunakuunga mkono na Wananchi wote wa Halmashauri ya Uyui songa mbele , asikutishe shetani wala mama mkwe wake  akikataa mtu kitu tutanyooshana hapa hapa," Alisisitiza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad