Mange Kimambi Awatetea Tuzo za Sinema zetu...Atoa Mfano wa Tuzo za Oscar Kuwapa Watoto Wadogo Tuzo....
0
February 25, 2019
Mwanaharakati Mange Kimambi ametia neno kuhusu Tuzo za Azam TV baada ya Wengi kulalamika kuwa tuzo wamepewa Watoto, Ameandika haya:
"Watanzania vitu vingine mnaweza kujifunza kwa kugoogle to. Hakuna tunzo kubwa za filamu duniani kama OSCAR na mara kibao tunaonana vitoto vidogo vinashindanishwa na wazee, mara nyingi hawashindi ila sometimes wanashinda.
Kuna kitoto cha miaka 10 kilishashinda OSCAR tunzo kubwa ya filamu duniani kwenye category ya muigizaji bora kikawashinda vikongwe wa filamu.
Tatizo watanzania wengi exposure ni ndogo mnooo. Mnashindwa hata kuelewa kuwa tunzo huwa zinaangalia kazi ya muigizaji kwa mwaka huo uliokwisha na sio kazi zao za miaka yote na ndio maana kitoto kidogo kinaweza kushinda tunzo. . Inabidi mjiulize why tuzo zipo kila mwaka na sababu ni kwamba wanaangalia kazi za mwaka mmoja TU!! .
Mmekaa mnalalamika tu, mmesahau Lupita Nyongo alishinda oscar ya best actress (supporting role)mwaka wake wa kwanza kabisa kuingia Hollywood na alishindanishwa na vikongwe kina Julia Roberts na akamshinda Julia Roberts. Sababu kubwa ni kwamba waliangalia kazi zao kwa mwaka wa 2013 tu wakaona kwa mwaka huo Lupita alimzidi Julia Roberts. Na movie aliyo act Lupita niliidharau sana ilipotoka niliiyonaga ya kizamani ila aliposhinda Lupita ndo nikaiangalia movie nzima.
So acheni upuuzi wa watoto kushindanishwa na watu wazima yani mnajionyesha mlivyo hamjaenda shule. Wengine eti ooh watoto wangewekwa category ya upcoming, jamani tuzo za filamu hazinaga category ya upcoming hizo huwa ni tuzo za mziki. .
Also hizi tuzo huwaga haziko perfect. Hata hapa marekani watu huwa wanalalamika kama Star anaempenda yeye hajashinda.
Na Wema aache utoto, ajifunze kukaa kimya. Anaruhusiwa kuumia ila sio kulalamika publicly,hata kama ni kweli kaonewa hatakiwi kusema sababu yeye alikuwa mshindani. Alitakiwa awaachie mashabiki wake ndio walalamike hapo kungekuwa na uzito Ila yeye kulalamika ni kama anawatia moto watu, VERY UNPROFESSIONAL. Huyo Johari ndo katia aibu jamani🙆🏽♀️. Mbona kina Monalisa wako very professional? .
La mwisho kabisa, Hamisa Mobetto aache kupania shughuli za watu sio kwa kupendeza kule utasema alikuwa nominee'