Marekani kununua mfumo wa Israel wa kujilinda dhidi ya makombora

Marekani kununua mfumo wa Israel wa kujilinda dhidi ya makombora
Jeshi la Marekani limetangaza mipango ya kutaka kununua na kujaribu mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Israel kwa jina Iron Dome.

Mfumo huo unaotumia rada na kutungua makombora kwa lengo la kukabiliana na tishio lolote umekuwepo tangu 2011.

Idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa mfumo huo utatumika kufanya majaribio huku ikitafuta mahitaji ya muda mrefu ya jeshi lake.


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametaja mauzo hayo kuwa mafanikio makubwa ya taifa lake.

''Hili ni dhihirisho jingine la kuimarika kwa ushirikiano wetu thabiti na Marekani, na onyesho kwamba Israel inazidi kupandisha hadi yake duniani, "taarifa yake iliendelea.

Ufanisi wake
Mfumo huo wa Iron Dome hufanya kazi kwa kufuatilia tishio lolote la shambulio kwa muda mfupi kupitia rada yake , kisha inachambua data kuhusu eneo litakaloathirika - kabla ya kuamua kurusha kombora litakalotungua shambulio hilo.

Maafisa wa Israel wanasema kuwa mfumo huo wa makombora unaoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote mbali na kusafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine una mafanikio ya hadi asilimia 90.

Unasemekana kuwa na uwezo wa kulinda mji mzima dhidi ya tisho lolote la angani na umetumiwa sana kutungua makombora yaliorushwa na wapiganaji wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza.


Ilichukua miaka kadhaa kuunda mfumo huo na ulitengezwa na kampuni ya ulinzi nchini Israel Rafael Advanced Defence Systems.

Marekani ilichangia sana katika uundaji wa mfumo huo, na baadhi ya vifaa vyake vinatoka kwa makampuni ya Marekani.

Katika taarifa, idara ya ulinzi nchini Israel ilisema kuwa ununuzi huo ulifanyika kutokana na mahitaji yake ya dharura ya jeshi la Marekani.

Ripoti zilivuja kuhusu ununuzi huo mwezi uliopita.

Kanali Patrick Seiber wa jeshi la Marekani amesema kuwa mfumo huo unachunguzwa na kujaribiwa ili kuwalinda wanajeshi wa Marekani waliotumwa katika mataifa ya kigeni.

Huku mfumo huo wa Iron Dome ukiwa umetumika na wanahewa wa Israel tangu 2011 na kuthibitisha uwezo wake katika vita, ilazima ibainike kuwa jeshi la Marekani litauchunguza kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa siku zijazo wa kujilinda , taarifa iliotolewa siku ya Jumatano ilisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad