Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu Februari 4, na ubalozi huo imesema inawakumbusha Wakenya kuendelea kuwa makini hasa wanapokuwa katika maeneo ya umma kama maduka makubwa ya manunuzi (malls), migahawa na sehemu za ibada.
“Kuweni makini na watu na vitu vinavyowazunguka na kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo mkiona vitendo msivyovielewa vinavyofanywa na raia wa kigeni lakini pia zingatieni ulinzi wenu binafsi,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inakuja zikiwa zimepita wiki tatu tangu kulipotokea shambulio la kigaidi lililofanywa na kundi la Al Shabab katika Hoteli ya Dusit eneo la Riverside Januari 15, mwaka huu.