Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo bado linamshikilia mtuhumiwa aliyesababisha kifo cha Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Tabora, Esther Gway wakati akijiokoa katika tukio la ubakaji, mara tu uchunguzi
utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda Nley amesema kuwa uchunguzi huo ukikamilika mtuhumiwa atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.
"Sisi kazi yetu kukamilisha uchunguzi tu, utakaohusisha mashuhuda pamoja na majirani wa eneo husika na baada ya hapo faili litakabidhiwa sehemu husika, kazi yetu itakuwa imeishia hapo", amesema Kamanda Nley.
Tukio hilo litokea, Januari 27, 2019 saa moja usiku katika eneo la Kariakoo mjini humo, ambapo mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake na kumkaba shingoni kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake.
Mauaji ya Askari wa JWTZ, Polisi wanachunguza
0
February 04, 2019
Tags