Mauaji ya Watoto Njombe, Matajiri Kuchunguzwa


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amezindua oparesheni maalum ya kuwasaka watuhumiwa wa mauaji ya watoto katika Mkoa wa Njombe kufuatia kuongezeka kwa mauaji ya watoto kwenye mkoa huo.


Kauli hiyo inakuja kufuatia kutokea kwa mauaji ya watoto 9 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole-Sendeka amebainisha kuwa ikitokea kwa tukio hilo familia nzima zitahusishwa na pamoja na viongozi wa eneo husika.

Ole Sendeka amesema "hata kama ulipigiwa simu tutaifuatilia simu yako, utatuunganisha na utatueleza mahusiano yako na huyo mtu na haya anayoyafanya ukijifanya kukataa tutakuunganisha kwenye mauaji ya watoto."

"Tungependa kuanza na  hawa ambao ni matajiri wanaoaminika walipata utajiri kwa njia ambazo si halali watatusaidia na tutawashika ili kuisaidia Jeshi la Polisi." ameongeza Ole Sendeka
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad